Browsing: Video Mpya

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewaagiza Mawaziri wanaohusika na utatuzi wa migogoro ya mipaka ikiwemo sekta za Ardhi, mifugo na Maliasili kwenda wilayani Mbarali mkoani Mbeya kushughulikia mgogoro unaodaiwa kuibuka hivi karibuni.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Mbarali Francis Mtega kutoa hoja kulitaka bunge kujadili kwa dharula mgogoro kwa taarifa kuwa mmoja wa wafugaji mifugo yake inashikiliwa na amedhamiria kujinyonga na hadi alipowasilisha hoja hiyo alikuwa bado anadhibitiwa na wananchi wanzake asitimize azma hiyo kwa sababu ya mifugo yake kukamatwa na kushikiliwa.

Akitoa majibu ya serikali kufuatia hoja hiyo Waziri Mkuu amewataka Mawaziri wote wa kisekta kwenda kutatua mgogoro huo haraka na kuwasilisha taarifa kamili ofisini kwake kesho saa mbili usiku.

Mama Janeth Magufuli, mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli, akifurahi na wanafunzi nyumbani kwake Chato leo Machi 18, 2023.

Mama Janeth amewaasa wanafunzi wasichana katika Shule za Msingi na sekondari nchini kote kujiepusha kabisa na mambo yanayoweza kuathiri maendeleo yao kimasomo.

Mama Magufuli amesema mambo mengi ya Kisasa hususan ya mitandao yamekuwa yakitengua mawazo chanya ya wasichana, na kuwashawishi waishi maisha ya mtandao ambayo mengi yao si maisha halisi.

“Kwa hiyo binti zango elekezeni akili, maarifa na juhudi katika masomo na sio mambo mengine yanayoweza kuathiri maendeleo yenu kimasomo kama vile mambo ya mitandao ambayo mengi sio yenye kuonesha maisha halisi”, alisema Mama Magufuli leo Machi 18, 2023 nyumbani kwake Chato, Mkoa wa Geita.

Mjane huyo wa Hayati Dkt. Magufuli alikuwa akiongea machache baada ya kutoa misaada ya taulo za wasichana na Baiskeli za magurudumu kwa Shule tatu za Sekondari za Wasichana zilizomo wilayani Chato.