Browsing: Video Mpya

Wafanyabiashara mkoani Mbeya wameiomba Serikali kuwapandisha vyeo maafisa wa Mamlaka ya mapato nchini kwa kigezo cha kuzalisha idadi kubwa ya walipa kodi badala ya kutumia kigezo cha kiwango kikubwa cha ukusanyaji mapato hali hiyo kimekuwa chanzo cha biashara nyingi kufa huku wakiomba kufanyika marekebisho ya sharia na kupunguza utitiri wa tozo ili kila mfanyabiashara awezi kulipa wa kwa hiari.

Hospitali ya Rufaa ya Mloganzila (MZRH) imeadhimisha Siku ya Saratani Duniani kwa dhamira ya kuimarisha huduma za uchunguzi, matibabu, na uhamasishaji wa jamii kuhusu ugonjwa wa saratani. Kupitia mikakati madhubuti, hospitali hiyo inajikita katika kuboresha upatikanaji wa huduma za uchunguzi wa mapema, matibabu bora, na elimu kwa jamii ili kuongeza uelewa na kupunguza maambukizi ya saratani.

Katika maadhimisho hayo, wataalamu wa afya wamehimiza wananchi kufahamu dalili za awali za saratani, kufanya uchunguzi wa mara kwa mara, na kuzingatia mtindo bora wa maisha kama njia ya kujikinga na ugonjwa huo. MZRH imeendelea kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya saratani kwa kuimarisha huduma zake za uchunguzi na matibabu, sambamba na kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta ya afya ili kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi wote.

Kaulimbiu ya mwaka huu inaangazia umuhimu wa usawa katika upatikanaji wa huduma za afya kwa watu wote, huku MZRH ikidhamiria kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya afya nchini.