Browsing: Video Mpya

SERIKALI YA TANZANIA KUWAFUTIA HADHI YA UKIMBIZI WAKIMBIZI WANAOISHI NCHINI.

Serikali ya Tanzania imesema inaenda kuwafutia hadhi ya ukimbizi Wakimbizi wanaoishi nchini baada ya kurejea kwa hali ya amani katika nchi zao baada ya hapo awali kuwepo kwa machafuko.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene huku jumla ya Wakimbizi 238,956 wanahifadhiwa hapa nchini ambapo Warundi ni 152,019,Wakongo ni 86,256 na mataifa mengine yakichangia idadi ya 681.

“Katika mkutano wa mwisho tulikubaliana kurejesha Wakimbizi 3000 kwa wiki,hata hivyo hadi tunakutana hapa hii leo 2025 ni Wakimbizi 3000 pekee waliorejea nchini kwao.Hili ni jambo ambalo lingepaswa kukamilika ndani ya wiki moja lakini limechukua takribani mwaka mzima,hatuwezi kuruhusu Hali hii iendelee hivi.” Alisema Waziri Simbachawene

KAULI MPYA KUTOKA CCM KYELA,FEDHA ZIMETOKA AU ZIMEUNGUA ,UCHUNGUZI UNAENDELEA.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya Bw.Elias Mwanjala amejitokeza hadhara kwa mara nyingine na kutoa kauli juu ya fedha ambazo alidai kuwa zimeteketea kwa moto wakati jengo la chama hicho lilipochomwa.

Bw.Mwanjala amesema kuwa ukweli wa fedha hizo kama zimeteketea kwa moto au kuchukuliwa na yeyote wameliachia vyombo vya ulinzi na usalama liendelee na uchunguzi.