Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amefungua rasmi Mkutano Mkuu wa 148 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha CICG, Geneva nchini Uswisi leo tarehe 24 Machi, 2024. Mkutano huo unatarajiwa kujadili Dhima Kuu ambayo ni “Matumizi ya Diplomasia ya Kibunge katika kuleta Amani na Maelewano Duniani”. Mkutano huo umehudhuriwa na Maspika wa Mabunge 48 na washiriki zaidi ya 1,500 na unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 27 Machi, 2024. Huu unakuwa Mkutano wake wa kwanza kuufungua tangu achaguliwe kuwa Rais wa IPU katika Uchaguzi uliofanyika Oktoba 27, 2023 nchini Angola.
Trending
- KERO ZAENDELEA KUTATULIWA MBEYA VIJIJINI, WANANCHI WATAKA MWENDELEZO.
- WAANDISHI WASAIDIZI KATA MKOA WA SINGIDA WAPIGWA MSASA
- *TANI ZA MBOLEA ZAMWAGWA MBEYA RC HOMERA NA SILINDE WATOA YA MOYONI*
- REGROW Yatoa Muongozo Mpya wa Kupokea na Kushughulikia Malalamiko ya Wananchi Wanaozunguka Hifadhi
- Mh Mahundi Aanza Ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya Kwa Gharama ya Zaidi ya Milioni 70
- Jinsi ya Kufikisha Malalamiko Kuhusu Mradi wa REGROW na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
- Serikali yagawa vishikwambi 350 kwa maafisa ugani Mkoani Mbeya
- RC. Homera azindua zahanati ya Sinai Kata ya Iwambi Jijini Mbeya