#MbeyaYetuTv #TRA_Songwe #TRA_Mbeya
Watu Watano wamefariki dunia kutokana na ajali ya gari aina ya Landcruiser yenye nambari za Usajili STL 8825 Mali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ambalo liligonga Lori aina ya FUSO yenye nambari za usajili T 586 ANE.
Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Hanseketwa Wilayani Mbozi Mkoani Songwe majira ya saa 11 alfajiri leo Agosti 23,2021.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Meneja Msaidizi Forodha Mkoa Songwe Omar Mzava amewataja marehemu kuwa ni Bernad Mushingi,ambaye ni Mfanyakazi wa Kituo cha Tunduma,Azaria Sivonike (Dereva wa Gari),Joel Mitondwa,Said Budi na Fahad Hassan wote wakiwa ni Wafanyakazi kituo cha Mbeya.
Trending
- Hii ndiyo Shule ya Sekondari Mbeya DAY!! inazidi kung’ara
- Viziwi waipongeza Serikali huduma za Afya, waomba alama itakayowatambulisha katika usafiri
- KAILIMA: WENGI WAJITOKEZA KUBORESHA AU KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARIO LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
- Bodi ya TASAC yaridhishwa utekelezaji wa maagizo kwa TPA
- TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM (2020-2025) MBUNGE VITI MAALUM MKOA WA MBEYA – MH. MAHUNDI
- Tulia Traditional Dances Festival 2024 Kurundima Mkoani Mbeya
- Uvumi kifo cha Muimbaji wa Injili Bonny Mwaitege Wazazi Waiomba Serikali kuchukua hatua
- Mtoto adaiwa kumuua baba yake mzazi kwa shambulio la mwili