Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

RAIS SAMIA NA RAIS MSTAAFU KIKWETE WAPONGEZWA KWA KUFANIKISHA USHINDI WA PROFESA JANABI KATIKA UCHAGUZI WA MKURUGENZI WA WHO KANDA YA AFRIKA

May 19, 2025

JK ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA MAREHEMU CLEOPA DAVID MSUYA HUKO MWANGA

May 19, 2025

INEC YATAKA VIONGOZI MIKOA 16 KUSHIRIKI KUONDOA WALIOKOSA SIFA

May 19, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • RAIS SAMIA NA RAIS MSTAAFU KIKWETE WAPONGEZWA KWA KUFANIKISHA USHINDI WA PROFESA JANABI KATIKA UCHAGUZI WA MKURUGENZI WA WHO KANDA YA AFRIKA
  • JK ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA MAREHEMU CLEOPA DAVID MSUYA HUKO MWANGA
  • INEC YATAKA VIONGOZI MIKOA 16 KUSHIRIKI KUONDOA WALIOKOSA SIFA
  • NI KILIO!!WAENDESHA BAJAJI NA WAKAZI MTAA WA JUHUDI ILEMI JIJINI MBEYA WALILIA MIUNDO MBINU BARABARA
  • NMB FOUNDATION KANDA NYANDA ZA JUU YATOA MAFUNZO KWA AMCOS KUWAWEZESHA WAKULIMA KAKAO KYELA
  • Wizi wa Bima Wafumuliwa, Serikali Yapanga Mashambulizi
  • INEC YAHIMIZA WANANCHI MIKOA 16 KUJITOKEZA UBORESHAJI DAFTARI AWAMU YA PILI
  • ZIARA KAMATI YA SIASA CCM MKOA MBEYA WATEMBELEA BWENIMRADI WA MIL 300 SEKONDARI SAGAMBI CHUNYA
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » DARAJA LA MINYUGHE, WILAYANI IKUNGI, SINGIDA KUFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI
Habari za Kitaifa

DARAJA LA MINYUGHE, WILAYANI IKUNGI, SINGIDA KUFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI

Mbeya YetuBy Mbeya YetuMarch 24, 2024No Comments7 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Serikali imekamilisha ujenzi wa daraja linalounganisha Kata ya Minyughe na Makilawa, katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida, lililokatika miaka mitatu iliyopita, na hivyo kuathiri shughuli za kiuchumi na upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu. Kukamilika kwa daraja hilo la chuma (Mibey Bridge) lenye urefu wa mita 30 lililogharimu zaidi ya Sh. Bilioni 1.6/-katika barabara ya Mtamaa-Minyughe hadi Mtavira, Wilayani Ikungi, litaenda kufungua fursa ya kiuchumi kwa wananchi wa kata hızo.Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA), Mkoa wa Singida, Mhandisi Ibrahim Kibasa, alisema kukamilisha uunganishaji wa vyuma kwa ajili ya daraja hilo, kumewezesha mto Minyughe kufunguka, na hivyo kutoa fursa kwa shughuli za uchukuzi kuendelea kati ya maeneo ya vijijini na makao makuu ya mkoa.Mhandisi Kibasa alisema kuwa, sasa wananchi wa kata tatu zinazounganishwa na daraja hilo, wataweza kuzikabili changamoto mbalimbali, zilizokwamisha shughuli zao, hususani wakati wa masika, kutokana na mto kufurika maji, kiasi cha kutishia usalama wao wakati wa kuvuka.

Ikungi

Serikali imekamilisha ujenzi wa daraja linalounganisha Kata ya Minyughe na Makilawa, katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida, lililokatika miaka mitatu iliyopita, na hivyo kuathiri shughuli za kiuchumi na upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu.

Kukamilika kwa daraja hilo la chuma (Mibey Bridge) lenye urefu wa mita 30 lililogharimu zaidi ya Sh. Bilioni 1.6/-katika barabara ya Mtamaa-Minyughe hadi Mtavira, Wilayani Ikungi, litaenda kufungua fursa ya kiuchumi kwa wananchi wa kata hızo.

Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA), Mkoa wa Singida, Mhandisi Ibrahim Kibasa, alisema kukamilisha uunganishaji wa vyuma kwa ajili ya daraja hilo, kumewezesha mto Minyughe kufunguka, na hivyo kutoa fursa kwa shughuli za uchukuzi kuendelea kati ya maeneo ya vijijini na makao makuu ya mkoa.

Mhandisi Kibasa alisema kuwa, sasa wananchi wa kata tatu zinazounganishwa na daraja hilo, wataweza kuzikabili changamoto mbalimbali, zilizokwamisha shughuli zao, hususani wakati wa masika, kutokana na mto kufurika maji, kiasi cha kutishia usalama wao wakati wa kuvuka.

” Sehemu ya fedha hizo ni bajeti mwaka ya mwaka huu ambapo tumejenga madaraja ikiwemo daraja hili la Minyughe,daraja hili limekuwa likiwasumbua wananchi takribani miaka mitatu na hivyo kukwamisha utekelezaji wa shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa Kata tatu pamoja na Mkoa wa jirani wa Tabora, katika wilaya ya Uyui, inayopakana na wilaya hii ya Ikungi, “alisema.
**
Aidha, Mhandisi Kibasa alisema, ujenzi wa daraja hilo umetokana na bajeti ya mwaka iliyotengwa, kiasi cha Sh. Bilioni 4.4/- katika wilaya ya Ikungi kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara na madaraja, katika halmashauri ya Wilaya hiyo.

Baadhi ya wananchi walioshuhudia kukamilika kwa kazi hiyo, akiwemo Bi. Elizabeth Bakari wa Kijiji cha Minyughe, na diwani wa Kata Minyughe , Mhe. Nelson Kiwesi, waliishukuru Serikali kwa mradi huo, ambao baada ya kukamilika, unakwenda kuondoa adha ya usafiri, hasa kwa wajawazito.

Bi. Elizabeth alibainisha kuwa, iliwalazimu kukosa huduma muhimu ikiwemo zile za afya katika kituo cha afya kilichopo ng’ambo ya pili, pia watoto wao kuhatarisha maisha wakati wa kwenda shule na kurudi nyumbani, hususani nyakati za masika, kutokana na mto Minyughe kufurika maji.

Alisema kukamilika kwa daraja hilo, sasa watoto wao hawatakosa masomo, wajawazito na wagonjwa wataenda kupata Huduma za matibabu kwenye kituo cha afya kilichopo ng’ambo ya daraja hilo pamoja na kufungua shughuli za usafirishaji wa mazao na watu.

“Kujengwa kwa daraja hili, ni mafanikio makubwa kwa watoto wetu waliolazimika kushindwa kuhudhuria vipindi vya masomo yao darasani. Serikali itaongeza mapato kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi , ikiwemo kilimo, na mali asili kupitia misitu, wazalishaji wamerahisishiwa mawasiliano kati ya upande mmoja na ule wa pili,” alisema.

Awali Mhandisi Mshauri Ebenezer Mollel, kutoka TARURA makao makuu, kitengo cha madaraja, alisema daraja hilo ni la tatu kujengwa hapa nchini, likitanguliwa na mengine lililopo Kihansi, huko Kilombero na lile la Mbuchi, kule Kibiti, mkoani Pwani.

Mhandisi Mollel alisema kuwa, madaraja hayo ni ya aina ya kipekee, hivyo kabla ya ujenzi hulazimika kuwapatia mafunzo Wahandisi wa TARURA na TANROADS, lengo likiwa kuwajengea uwezo, kwa ajili ya kupata ujuzi na utaalamu zaidi kuweza kumudu majukumu yao, kulingana na kukua kwa teknolojia, huku wahandisi walioshiriki mafunzo hayo, wakifikia 42.

Kwa mujibu wa mhandisi Mollel, teknolojia ya daraja hilo ni ya kipekee, kutokana kujengwa likiwa ng’ambo ya pili, na baada ya kukamilika husukumwa hadi sehemu yake, kuunganisha kingo mbili, na kuwa tayari kwa ajili ya matumizi ya kivuko.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

RAIS SAMIA NA RAIS MSTAAFU KIKWETE WAPONGEZWA KWA KUFANIKISHA USHINDI WA PROFESA JANABI KATIKA UCHAGUZI WA MKURUGENZI WA WHO KANDA YA AFRIKA

May 19, 2025

JK ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA MAREHEMU CLEOPA DAVID MSUYA HUKO MWANGA

May 19, 2025

INEC YATAKA VIONGOZI MIKOA 16 KUSHIRIKI KUONDOA WALIOKOSA SIFA

May 19, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024171

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202481

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202560

DKT. TULIA ATOA MSAADA WA VIPAZA SAUTI MSIKITI WA MASJID BI FATMA NZOVWE JIJINI MBEYA

March 29, 202457
Don't Miss
Habari za Kitaifa

RAIS SAMIA NA RAIS MSTAAFU KIKWETE WAPONGEZWA KWA KUFANIKISHA USHINDI WA PROFESA JANABI KATIKA UCHAGUZI WA MKURUGENZI WA WHO KANDA YA AFRIKA

By Mbeya YetuMay 19, 20251

Na Mwandishi `Maalumu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,…

JK ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA MAREHEMU CLEOPA DAVID MSUYA HUKO MWANGA

May 19, 2025

INEC YATAKA VIONGOZI MIKOA 16 KUSHIRIKI KUONDOA WALIOKOSA SIFA

May 19, 2025

NI KILIO!!WAENDESHA BAJAJI NA WAKAZI MTAA WA JUHUDI ILEMI JIJINI MBEYA WALILIA MIUNDO MBINU BARABARA

May 19, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

RAIS SAMIA NA RAIS MSTAAFU KIKWETE WAPONGEZWA KWA KUFANIKISHA USHINDI WA PROFESA JANABI KATIKA UCHAGUZI WA MKURUGENZI WA WHO KANDA YA AFRIKA

May 19, 2025

JK ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA MAREHEMU CLEOPA DAVID MSUYA HUKO MWANGA

May 19, 2025

INEC YATAKA VIONGOZI MIKOA 16 KUSHIRIKI KUONDOA WALIOKOSA SIFA

May 19, 2025
Most Popular

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024171

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202481

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202560
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.