Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linapenda kutoa taarifa ya kifo kilichohusisha
watu watano wa familia moja huko Wilaya ya Chunya.
Ni kwamba mnamo 29.12.2024 saa 8:30 usiku katika Kitongoji cha Nkangi
kilichopo Kijiji cha Isangawana, Kata ya Matwiga, Tarafa ya Kipembawe,
Wilaya ya Chunya, watu watano wa familia moja ya Masiganya Scania [39]
mfugaji, mkazi wa Nkangi walifariki dunia baada ya kupigwa radi kwenye
kambi ya kuchungia Ng'ombe wakati wakiwa wamelala.
Waliofariki katika tukio hilo ni Balaa Scania [28], Kulwa Luweja [17], Masele
Masaganya [16], Hema Tati [10] na Manangu Ngwisu [18] wote wakazi wa
Kijiji cha Nkangi. Aidha, katika tukio hilo watu wengine watano walijeruhiwa
ambao ni Gulu Scania [30], Manyenge Masaganya [13], Seni Solo [13],
Paskali Kalezi [16] na Huzuni Kalezi [19] wote wakazi wa Kijiji cha Nkangi.
Chanzo cha tukio hilo ni mvua kubwa iliyonyesha usiku ikiambatana na radi
hivyo kusababisha vifo vya watu watano na wengine watano kujeruhiwa.
Majeruhi walikimbizwa katika Kituo cha Afya Isangawana kwa matibabu na
walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani baada ya hali zao kuwa nzuri.
Trending
- Siri Yangu Ya Kuvutia Wateja Hadi Dukani Kwangu, Sasa Biashara Imekuwa Tajiriba Kubwa
- Nyuki wa Ajabu Wamfukuza Mwanamke Kwa Aibu Kubwa Kutoka Kwa Nyumba ya Mpenzi
- Kutoka kuchunga ng’ombe hadi kushinda Sh27.4 milioni ya jackpot
- WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI
- MA-EMSII MBEYA WALIA NA UTITIRI WA TOZO NA KODI KATIKA KAZI ZAO,DC ITUNDA AAHIDI KUTAFUTIA SULUHU
- Wazazi Wafichua Mbinu Walizotumia Kuwalinda Watoto Wao Dhidi ya Jicho Baya na Uovu
- MH. MICHAEL MAKAO ALIVYOREJESHA FOMU YA UDIWANI KATA RUJEWA AAHIDI KUENDELEZA ALIPOISHIA
- Mwanamke Afumaniwa Akipika Chakula Usiku kwa Mtu Asiyeonekana, Jirani Atoa Neno