Wakazi wa jiji la Mbeya walishtushwa na tukio lisilo la kawaida lililotokea katika mtaa wa Forest, ambapo mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Richard aliripotiwa kushindwa kutembea ghafla baada ya kutoka nyumbani kwa mwanamke anayedaiwa kuwa mpango wake wa kando.
Tukio hilo liliwavutia watu wengi na kuzua mijadala mikali kuhusu uaminifu kwenye ndoa na nguvu za kiroho.
Kwa mujibu wa mashuhuda, Richard alikuwa ameonekana akiingia nyumbani kwa mwanamke huyo mchana wa saa nane. Ilielezwa kuwa alikuwa amevalia mavazi rasmi, akionekana mwenye furaha.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya kuingia, vilisikika vilio vya maumivu na kelele kutoka ndani ya nyumba hiyo.
Ilibidi majirani waingilie kati, na ndipo walipomkuta Richard akiwa amelala sakafuni, miguu yake ikiwa haina uwezo wa kusimama, huku akilia kwa uchungu na kumtaja mke wake wa ndoa kwa sauti ya huzuni. Soma zaidi hapa