Diwani wa Kata ya Ilomba, Ndg. Noah Edson Mwakisu, leo amerejesha fomu za kuwania Umeya wa Jiji la Mbeya kupitia CCM. Akizungumza katika Ofisi za CCM Mbeya Mjini, Mwakisu alisema anagombea nafasi hiyo ili kulipa jiji mwelekeo mpya wa maendeleo, akisisitiza umuhimu wa uongozi wenye maono, ushirikiano na uwajibikaji.
Mwakisu alisema Mbeya ina fursa kubwa za kimaendeleo kutokana na mazingira na jiografia yake, hivyo inahitaji kiongozi anayeendana na mahitaji ya kizazi cha sasa, hususan vijana ambao ndio nguvu ya uchumi wa jiji. Aliomba sapoti na baraka za wananchi, akiahidi kulifanya jiji hilo mfano wa kuigwa endapo atapewa dhamana.
Kurejesha fomu hizo kunamweka rasmi katika kinyang’anyiro cha ndani ya CCM cha kuwania Umeya wa Jiji la Mbeya mwaka huu.
Trending
- Mbinu ya kupata faida katika biashara ya samaki, uvuvi
- WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUZUIA HATI YAKE
- Mgombea Umeya Jiji la Mbeya, Noah Mwakisu Arejesha Fomu; Aahidi “Ukombozi wa Jiji”
- MVUA ILIYONYESHA LUMBILA IWAMBI MBEYA MITARO YAFURIKA MAKAZI YA WATU YAJAA MAJI BIASHARA ZASIMAMA
- Afanikiwa kuoa baada ya kuvunja vifungo vya ukoo!
- MWAKIPESILE: ”YALIYOJIRI OKT 29 YAMETUUMIZA,TUMUUNGE MKONO RAIS,WAZIRI MKUU MWIGULU NI MZALENDO”
- Hadi nilishindwa kujiamini nikiwa faragha!
- Rais Samia Ahoji Kilio cha Vijana: “Walikuwa Wanaidai Haki Ipi?”

