Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Ndg. Salim Abri Asas, ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Mradi wa Soko la Matola jijini Mbeya, akieleza kuwa haiwezekani kukamilika mwezi Mei kama ilivyopangwa.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi katika maadhimisho ya miaka 49 ya CCM, Asas alisema mradi unasuasua licha ya fedha kuwepo. Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Mhe. Dk. Mohamed Issa, alimweleza kuwa mkandarasi ameshindwa kusimamia fedha za mradi ipasavyo.
Kwa upande wake, MNEC Ndg. Ndele Mwaselela alisema idadi ndogo ya wafanyakazi na kasi ndogo ya ujenzi ni sababu kuu zinazoathiri ukamilishaji wa mradi.
Ndg. Asas alisema atawasilisha taarifa ya kweli kwa mamlaka husika, akisisitiza kuwa hatakubali kutoa taarifa ya kukamilika kwa mradi wakati hali halisi ni tofauti.
Trending
- Mradi wa Soko la Matola Wakwama, Meya na MNEC Wakanusha Kukamilika Mei
- JK KWA MFALME MSWATI III KUJADILI UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA KWA NCHI WANACHAMA WA ECSA
- Halmashauri Yaipongeza Mbeya UWSA Kwa Mradi wa Maji, Asema Utakuza Uwekezaji
- Mpango wa Maendeleo 2026/27: Kasaka Apongeza Mafanikio, Aomba Maboresho
- Msafara Wasimama Soweto, Mbunge Mwalunenge Aamuru TANROADS Kuondoa Dimbwi la Miaka 3 Mara Moja
- CCM Miaka 49: Mbunge wa Mbarali Akabidhi Mashuka Kituo cha Afya Utengule
- Dkt. Tulia Ackson Atoa Msaada wa Vifusi Roli 10 kwa Ukarabati wa Barabara ya Chanyasi
- TGNP na CARE Watoa Mafunzo ya Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa Jamii Mbeya

