#MbeyaYetuTv #TRA_Songwe #TRA_Mbeya
Watu Watano wamefariki dunia kutokana na ajali ya gari aina ya Landcruiser yenye nambari za Usajili STL 8825 Mali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ambalo liligonga Lori aina ya FUSO yenye nambari za usajili T 586 ANE.
Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Hanseketwa Wilayani Mbozi Mkoani Songwe majira ya saa 11 alfajiri leo Agosti 23,2021.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Meneja Msaidizi Forodha Mkoa Songwe Omar Mzava amewataja marehemu kuwa ni Bernad Mushingi,ambaye ni Mfanyakazi wa Kituo cha Tunduma,Azaria Sivonike (Dereva wa Gari),Joel Mitondwa,Said Budi na Fahad Hassan wote wakiwa ni Wafanyakazi kituo cha Mbeya.
Trending
- Ulinzi Mkali Waimarishwa Kuelekea Krismasi na Mwaka Mpya 2026 – Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
- MSHTUKO MBEYA: MTOTO DARASA LA SABA AUAWA KWA KIPANDE CHA MTI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MAYAI
- Nilipoteza Amani Bila Sababu Inayoonekana Ufafanuzi wa Kienyeji Ulinipa Mwanga
- MH. MAHUNDI AWAHIMIZA VIJANA KUISHI KWA MISINSI YA UWAJIBIKAJI NA UTU
- Familia Yetu Ilikosa Baraka ya Utulivu Tulipoelewa Chanzo, Njia Ikafunguka
- Tulikaa Ndoa Bila Amani Mazungumzo Moja Yalibadili Mwelekeo Wetu
- Maumivu ya Ghafla Yalinifanya Nidhani Ni Mwisho, Baadaye Nikagundua Mawe ya Figo Yanatibika Kwa Mitishamba
- Tazama alichoimba Dkt. Tulia Ackson Atoa sadaka kwa kaya 13 zisizo na uwezo kata ya Ilemi
