AJALI YA GARI KUGONGA MAGARI MATATU NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI.Ni kwamba mnamo tarehe 16.08.2022 majira ya saa 02:00 asubuhi huko maeneo ya Inyala Pipeline, Kijiji cha Shamwengo, Kata ya Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya – Njombe, Gari lori lenye namba za usajili T.387 DFJ lenye tela namba T.918 DFE aina ya Dayun likiendeshwa na Dereva MUHSIN GUMBO, Mkazi wa Dar es Salaam mali ya kampuni ya Evarest Frech Ltd likiwa na kontena la mchanga likitokea Mbeya liligonga kwa nyuma Gari T.966 DUQ aina ya Fuso basi mali ya kampuni ya Super Rojas likitokea Mbeya kuelekea Njombe likiendeshwa na ALEX MGIMBA [51] Mkazi wa Jijini Mbeya na kisha kugonga Gari T.836 DRE Mitsubish Benz iliyokuwa ikiendeshwa na NEDIM PREMJI, Mkazi wa Dar es Salaam na kisha kugonga Gari linguine T.342 CHG/T.989 CGS Scania iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika na kusababisha vifo vya watu 19 kati yao wanaume ni 12, wanawake 06 na mtoto 01. Aidha katika ajali hiyo majeruhi ni 10 kati yao wanaume ni 07, wanawake ni 02 na mtoto 01.Chanzo cha ajali ni Gari kufeli breki kwenye eneo lenye mteremko mkali na kisha kugonga magari mengine. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na Hospitali ya Igawilo. Imetolewa na:Ulrich Matei – SACPKamanda wa Polisi,Mkoa wa Mbeya.
Trending
- PADRE ”AWAPIGA MADONGO” WADOEZI WA CHAKULA CHA WAFIWA MSIBANI
- PADRE KATOLIKI IGURUSI ASIMULIA ALIVYOTELEKEZEWA MAITI NA WAUMINI KANISANI
- DKT TULIA ALIVYOGUSWA NA KIFO CHA MZEE MWANSASU NSONYANGA
- Jinsi ya Kufikisha Malalamiko Kuhusu Mradi wa REGROW na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
- Mamlaka ya Maji Mbeya Yachukua Hatua Kuwafikia Wakazi wa Gombe Kusini Kutatua Tatizo la Maji
- WATU MASHUHURI WAHUDHURIIA MAZISHI YA MZEE MWANSASU NSONYANGA ,PADRE SIMON ATOA UJUMBE MZITO
- MRADI WA REGROW KUCHOCHEA UCHUMI WA WANANCHI WANAOPAKANA NA HIFADHI KUSINI MWA TANZANIA
- Betty (Rehema) Fwelefwele Kalala wa Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara, Anatafuta Baba Yake Mzazi Aitwaye Method Kapinga