Author: Mbeya Yetu

Wananchi wa Jimbo la Paje lililopo katika Wilaya ya Kusini,Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika moja ya vituo kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,leo tarehe 7 Oktoba,2024. Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Zanzibar umeanza leo Oktoba 07 hadi Oktoba 13, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.  Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari (kushoto) leo Oktoba 07, 2024 ametembelea vituo vya kuandikishia Wapiga Kura katika Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar…

Read More

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYAUWSA)imeandaa maadhimisho ya huduma kwa wateja yanayofanyika oktoba 7,2024 hadi oktoba 11,2024 yenye lengo la kuenzi huduma zinazotolewa na Mamlaka sanjari na wanayopata wateja wao.

CPA Gilbert Kayange amesema hitaji la upatikanaji wa maji Jijini Mbeya na Mbalizi ni lita 90m wakati upatikanaji wa maji kwa sasa ni 72.5m kwa siku.

Aidha amesema Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira imetoa ofa kwa wadaiwa wote waliokatiwa maji kuanzia oktoba mosi hadi oktoba 30 watapaswa kulipa nusu ya deni Ili kurejeshewa huduma ya maji.

Pamoja na utaratibu huo Kayange amesema Mamlaka itatoa elimu kwa wateja wao ili wajue haki zao pia wajibu wao.

Read More

  Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk leo tarehe 04 Oktoba, 2024 ametembelea na kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya ya Wete na Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba yanayofanyika kwa siku mbili. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa sita wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao utajumuisha mikoa mitano ya Zanzibar. Uboreshaji wa Daftari kwenye maeneo hayo utaanza Oktoba 07 hadi Oktoba 13, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa…

Read More