Author: Mbeya Yetu

23 Mei 2024, jijini Tartu nchini Estonia, Mheshimiwa Injinia Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na TEHAMA, alifanya kikao na uongozi wa Taasisi isiyo ya kibiashara ya e-Governance Academy (eGA) ya serikali ya Estonia. Mkutano huo ulifanyika kandokando mwa Kongamano la 10 la Utawala wa Mtandao (10th e-Governance Conference) ambalo lilibeba kauli mbiu ya “Unlocking Digital Success”. eGA ni kituo cha umahiri kilichojikita kwenye mapinduzi ya kidijitali ya jamii ndani ya Estonia na duniani kote. Kituo hicho kinawakutanisha wataalamu wabobezi mbalimbali wenye weledi wa mambo ya kidijitali kutoka Estonia. Katika kikao hicho, eGA iliongozwa na Mkurugenzi Mkuu…

Read More

Mkuu wa Ofisi ya Tume ya Ushindani (FCC)Kanda ya Nyanda za Juu Dickson Mbanga amewataka wananchi wa Mikoa hiyo kujitokeza katika maonesho ya Biashara ya Mbeya Expro 2024 ili wajifunze utambuzi wa bidhaa bandia zinazozagaa mitaani kwa lengo la kumlinda mlaji.

Mbanga ametoa rai hiyo katika Banda la Tume ya ushindani wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda hilo.

Baadhi ya wananchi waliotembelea banda hilo wakiwemo Theresia Chengula na Happy Mkokwa ambao wamesema maonesho hayo yamewajengea uelelewa kwani hivi sasa wanao uwezo wa kuzitambua bidhaa bandia.

Read More

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Kanda ya Nyanda za Juu ni miongoni mwa Taasisi za Umma zinazoshiriki maonesho ya Biashara ya Mbeya City Expro 2024 yanayoendelea katika Soko la Zamani la Uhindini Jijini Mbeya yaliyoanza mei 22,2024 na yatatamatika mei 30,2024. Meneja wa Kanda Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Kanda ya Nyanda za Juu Josiah Murunya amesema lengo la Baraza ni kutoa elimu kwa jamii kupitia maonesho hayo.Kanda ya Nyanda za Juu inajumuisha Mikoa ya Mbeya, Njombe, Songwe na Rukwa. Mmoja wa washiriki mkazi wa VETA Jijini Mbeya Agrey Kiwale aliyetembelea Banda…

Read More

Maonesho ya Biashara ya Mbeya City Expo 2024 yanaendelea kung’ara jijini Mbeya, yakikusanya washiriki kutoka sekta mbalimbali za biashara na huduma. Maonesho haya yamekuwa yakifanyika kwa lengo la kuimarisha uchumi wa kanda ya nyanda za juu kusini na kuvutia wawekezaji wapya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, alifungua rasmi maonesho haya akisisitiza umuhimu wake katika kukuza biashara za ndani na kimataifa. Katika hotuba yake, alieleza jinsi maonesho haya yanavyotoa fursa kwa wajasiriamali wa ndani kujifunza na kubadilishana uzoefu na wenzao kutoka maeneo mbalimbali​

Read More