Author: Mbeya Yetu

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza na waandishi wa habari Mjini Unguja, Zanzibar, leo tarehe 15 Mei, 2024, ambapo ametangaza kuwa uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika tarehe 01 Julai, 2024. (Picha na INEC). Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele (katikati) akizungumza na waandishi wa habari Mjini Unguja, Zanzibar, leo tarehe 15 Mei, 2024, ambapo ametangaza kuwa uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika tarehe 01 Julai, 2024. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Bw.…

Read More

Mkaguzi kata ya Lwenzera Wilaya ya Geita Mkoani Geita amewataka Walimu Wa Shule ya Sekondari Bugando Kufuata Maadili ya Kazi huku akiwataka kutambua kuwa Jamii inawategemea katika kuwafundisha na kutoa malezi Mema kwa Wanafunzi. Hayo yamebainishwa na Mkaguzi wa Kata hiyo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Pili Kulele wakati alipotembelea Shule hiyo ambapo amewaomba walimu kujikita katika kuwafundisha wanafunzi na kutoa malezi mema ili wawe msaada katika Jamii na kata hiyo kwa ujumla. Mkaguzi kulele amewasihi walimu hao na kuwaambia kuwa kumekuwepo na baadhi ya walimu wasiofuata maadili ya kazi hiyo na kuchafua taswira nzuri na historia nzuri iliyowekwa na…

Read More

Mratibu wa Kambi ya Madktari bingwa wa rais samia kutoka wizara ya afya Bi. Jackline Ndeshau ameeleza kuwa wamejipanga kuhudumia wananchi wote watakaojitokeza kipindi cha siku 5 za kambi hii mkoani songwe katika maeneo 5 na kutoa rai kwa wananchi kujitokeza kutumia fursa hiyo ambapo lengo lake ni kusogeza huduma za afya karibu na jamii, kuongezea ujuzi wataalamu wa afya waliopo katika vituo husika vilevile kupunguza gharama za kwa wananchi kuzifwata huduma hizo za kibingwa nje ya kituo husika.
Amesema kambi ya madaktari bingwa na bobezi wa Rais Samia wanategemea kutoa huduma za afya kwa watoto na watoto wachanga, huduma za upasuaji, huduma za afya ya uzazi, wajawazito na magonjwa ya wanawake, huduma za ganzi na usingizi na huduma ya magonjwa ya ndani mkoani songwe kwa siku tano katika hospitali za wilaya ya Tunduma, Itumba, Vwawa, Momba na hospitali ya halmashauri wilaya ya Songwe

Read More

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprica Mahundi (Mb) amesema Serikali inatarajia kujenga jumla ya minara 15 katika kata mbalimbali za Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Naibu Waziri Maryprisca amesema hayo tarehe 13 Mei, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Isseke, Wilaya ya Manyoni akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa mnara wa mawasiliano unaojengwa na kampuni ya simu ya Airtel kwa kushirikiana na UCSAF.
Amesema minara hiyo 15 itajengwa katika kata za Isseke, Makanda, Makutupora, Maweni, Mitundu, Mkwese, Mwamagembe, Nkonko, Rungwa, Sanjaranda, Sanza, Saranda, Sasajila na Sasilo ili kuimarisha huduma za mawasiliano.
Akizungumzia Mnara wa Isseke unaoendelea na ujenzi,
Mhandisi Maryprisca amesema umeigharimu Serikali jumla ya
Tsh. 116,500,000/- ambapo asilimia 70 ya fedha hizo ambazo ni Tsh. 81,550,000/- tayari zimeshalipwa na UCSAF kwa Airtel.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa mara huo na kuanza kutoa huduma ya Mawasiliano kutawasaidia wakazi wa Vijiji vitakavyofikiwa kwa kuboresha shughuli za kiuchumi na
kupata mawasiliano kwa haraka hususan taarifa muhimu za masoko.
Amesema mawasiliano ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi wa Manyoni kwani yatasaidia pia kuokoa muda wa kufunga safari ili kupata huduma umbali mrefu na kurahisisha huduma za kutuma na kupokea pesa ambazo sasa zitatanyika majumbani.

“Tunaishukuru sana kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na UCSAF, kwa kuchukua uamuzi huu wa kuipa
Wilaya ya Manyoni kipaumbele na kuamua kufikisha huduma za mawasiliano ya uhakika kwa wakazi zaidi ya 6,900 wa vijiji
Maryprisca.

Read More

Na. Mwandishi Wetu, Zanzibar Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imepitisha Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024 na Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za Mwaka 2024 ikiwa ni hatua muhimu katika kuzitafsiri sheria zilizotungwa na Bunge hivi karibuni.   Sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazohusu uchaguzi ni Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 na Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya Mwaka 2024.   Kanuni hizo zilizopitishwa leo tarehe 11 Mei,…

Read More

Waziri Mkuu Kasssim Majaliwa leo Mei 12, 2024 ametembelea shamba la Mkulima zao la Kakao Clement Msalangi lililopo kijiji cha Mababu, Wilayani Kyela Mei 12, Akizungumza baada ya kulitembelea Mheshimiwa Majaliwa amewataka wakulima wa zao hilo wajisajili na watambue idadi ya miche waliyonayo na ukubwa wa mashamba yao ili wakati Serikali ikitoa ruzuku kila mkulima anufaike na kuiwezesha Serikali kujua ni tani kiasi gani itazalishwa. Aidha, Waziri Mkuu amewataka wakulima na viongozi wa AMCOS wasimamie ubora zao la Kakao na kuzitumia fedha wanazopata baada ya mauzo kujiletea maendeleo katika maeneo yao.

Read More