Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- Viongozi 11 wa CHADEMA washikiliwa na Polisi Mkoa wa Songwe
- ZIARA YA NAIBU WAZIRI MAHUNDI ZANZIBAR
- Jinsi ya Kufikisha Malalamiko Kuhusu Mradi wa REGROW na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
- Naibu Waziri Mhandisi Maryprisca Mahundi Akagua Hali ya Mawasiliano Kisiwani Kojani, Pemba
- Inauma sana: Mtoto wangu kaenda chuo kikukuu katumbukia katika umalaya na dawa za kulevya
- WALIOKUWA WANAENDA KUMZIKA NEEMA ALIYEFIA KARIAKOO WAPATA AJALI, MMOJA AJARIKI
- Mbunge Jimbo la Busokelo Mh Mwakibete Serikali ya chama cha Mapinduzi imeitendea haki mkoa wa Mbeya
- Mbunge wa Kyela Ally Jumbe Kinanasi Awakumbusha wana Mbeya
Author: Mbeya Yetu
Jina langu ni Marko kutoka Dodoma, Tanzania, niliwahi kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu sana lakini sikupata suluhisho kwa kupata matibabu kwa wakati ule kwani wazazi wangu hawakuwa na uwezo wa kifedha. Nilipata shida sana sikuweza kuendelea na masomo kwasabau ya ugonjwa wangu uliokuwa ukinisumbua miaka mingi sana, lakini siku zilivozidi kwenda nilitamani nije kuwa kawaida kama wengine wanavyofrahia maisha yao na familia zao. Mimi na wazazi wangu nalitamani nije nipone huo ugonjwa ili niweze kusaidia wazazi wangu, siku moja nilipigiwa simu na rafiki yangu ambaye yeye anaishi huko Zanzibar. Nilisoma nae darasa moja tangu tulivyoachana hatukuwahi kuonana,…
Jina langu ni Samsoni kijana wa miaka 26, naishi Dar es Salaam, Tanzania, nikiwa kazini kwangu nilikuwa na mahusiano na binti ambaye yeye alikuwa akifanyia kazi zake Morogoro. Baada ya mwezi mmoja nilimpigia simu kuwa mwezi unaofata nitaenda kwake, siku ilivyofika nikijiandaa ili nifike kwake, lakini hakuweza kupokea simu yangu nikajiuliza kimempata nini mpaka hapokei simu yangu?. Nikasema hapa lazima kuwa na kitu, sikutaka kubaki, nilifika hadi kwake, kabla sijaingia ndani nilisikia sauti ya mwanaume, nikaingia kimya kimya bila yeye kujua nilifika hadi chumbani kwake. Nilichokikuta sikuamini nilimfumania yeye pamoja na Bosi wake, niliumia sana, kuna akili ikawa inanituma, sijui…
Na Mwandishi wetu, Dodoma Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wameendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa TEHAMA wa taasisi hiyo. Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Bw. Kailima Ramadhani, amesema kuwa Mafunzo haya ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usimamizi wa teknolojia ya habari na mawasiliano katika taasisi hiyo. Amesema Tume inajitahidi kuwekeza katika TEHAMA, hasa kwa kutumia vifaa vya BVR (Biometric Voter Registration) katika uandikishaji wa wapiga kura, pamoja na mifumo ya kusimamia daftari, matokeo, wagombea, na waangalizi wa…
Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi.
Timu maalumu ya kupambana na makosa ya mtandao kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano TCRA wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 20 wakiwemo raia 04 wa Nchi jirani kwa makosa ya kuingilia mifumo ya mawasiliano.
Akitoa taarifa hiyo leo Oktoba 29, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti Mkoani Arusha kwa mwezi huu wa Oktoba 2024.
SACP Masejo amebainisha kuwa watuhumiwa 16 kati ya waliokamatwa ni mawakala wa kusajili laini za mitandao ya simu ambao wanasajili laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya Taifa NIDA vya watu wengine bila ridhaa zao na kisha kuuza kwa wahalifu hao ambao huzitumia kuingilia mifumo ya mawasiliano na kufanya uhalifu.
Aidha katika ufuatiliaji walibaini kuwa laini nyingi wameziuza kwa raia hao 04 wa Nchi Jirani ambao walikutwa na mitambo ya mawasiliano aina ya Simbox, Laini mbalimbali za mitandao ya simu, kompyuta mpakato, komptyuta, simu za mikononi, invetor solar na betri za solar.
Kamanda Masejo amesema upelelezi wa shauri hilo umekamilika, na taratibu nyingine za kisheria zinafuata.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linatoa wito kwa watu wanaosajili laini za simu ambao sio waaminifu wanaotumia vitambulisho vya Taifa vya watu wengine kusajili laini na kuuza kwa watu wengine kuacha mara moja kwani wataendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi yao.
Halikadhalika limetoa rai kwa wamiliki wa nyumba kuwa makini na wapangaji wanaowapangisha katika nyumba zao, kwani baadhi ya wahalifu hutumia nyumba hizo kufanya vitendo vya kihalifu.
Sambamba na hilo Jeshi la Polisi Mkoani humo limewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kila mara wa kupiga namba *106# ili kujua namba zilizosajiliwa kupitia vitambulisho vyao vya NIDA ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.
Jina langu ni Mama Jesca kutokea Mwanza, Tanznia, nina watoto watatu, wawili wapo shule, mwingine yupo darasa la sita, mdogo wake yupo darasa la nne. Wanangu kila walipokuwa wakifanya mtihani walikuwa wanafeli. Jioni wakirudi kutoka shule nikawa nawapa mifano ya watoto wawili. Wanafunzi wawili wanaotoka kufanya mtihani unaofanana, wote wanatoka wamefurahi kwenye chumba cha mtihani. Mmoja anamwambia mwenzie mtihani huu ulikuwa mwepesi sana lakini kwenye matokeo lolote linaweza kutokea tunaweza tusipate B. Mwenzake akamjibu; wewe unaongea nini wewe!, mtihani huu lazima tupate B, lazima tena nina uhakika kabisa. Matokeo yalipobandikwa yalionesha wote wana alama ‘D’ ambayo ni sawa na kufeli,…
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Shirikisho la Urusi, Bw. Maxim Reshetnikov na kujadiliana naye masuala mbalimbali yakiwemo yanayogusa biashara, kilimo, usafirishaji, elimu, nishati na utalii.
Akizungumza na Waziri Reshetnikov leo (Jumatatu, Oktoba 28, 2024) ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amemhakikishia Waziri huyo kwamba Tanzania ni mahali pazuri pa kufanya biashara kwa kuwa ni nchi tulivu na Mwenyezi Mungu ameiweka mahali pa kimkakati pa kuweza kufanya biashara.
“Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipambanua kufanya maboresho kwenye biashara kati ya Tanzania na nchi marafiki, Urusi ikiwemo. Kupitia ziara hii, nina uhakika mtapata maelezo mazuri ambayo yatawatia moyo wa kuiamini Tanzania kwamba ni mahali pazuri pa kufanyia biashara,” amesema,
Akielezea kuhusu fursa zilizopo nchini, Waziri Mkuu amesema Tanzania inapakana na bahari yenye bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga. “Ina maziwa ya Victoria, Tanganyika, Nyasa na yenye bandari kadhaa. Ziwa Victoria kuna bandari kule Kagera, Mwanza na Musoma. Ziwa Tanganyika kuna bandari za Kigoma, Kabwe na Kasanga na Ziwa Nyasa kuna bandari za Mbambabay na Kyela.”
Amesema bandari hizo zimeunganishwa na barabara, reli ya kati, TAZARA, reli ya SGR na vyote vinaenda hadi nje ya nchi ili kurahisihwa usafirishaji wa bidhaa. “Tunao usafiri wa uhakika kutoka Dar es Salaam hadi Kapiri-Mposhi, Zambia ambako bidhaa zinachukuliwa na kupelekwa nchi nyingine. Pia SGR itakapokamilika, itawezesha kufikisha mizigo hadi Rwanda, Uganda na Congo.”
Kuhusu kilimo, Waziri Mkuu amewakaribisha wafanyabiashara kutoka Urusi waje kuwekeza kwenye kilimo kwa kuwa Tanzania ina eneo kubwa la ardhi na lenye rutuba kwa ajili ya shughuli za uzalishaji. “Malengo ya Tanzania ni kuona tunakuwa kitovu cha uzalishaji wa chakula barani Afrika.”
Ametumia fursa hiyo kumweleza faida mbalimbali za kuwekeza Tanzania kubwa ikiwa ni uhakika wa wateja kwa bidhaa zao kwani yenyewe ina wakazi zaidi ya milioni 61, ukanda wa Afrika Mashariki una watu zaidi ya milioni 300 na pia nchi za SADC ambako Tanzania ni wanachama, una uhakika wa soko la watu zaidi ya milioni 300.
“Tanzania ni lango kwa nchi nane zinazotuzunguka na mbili ziko mbioni kujiunga. Nchi hizo ni Kenya, Uganda, DRC, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi na Msumbiji. Kuna nchi mbili za Comoro na Sudan Kusini ambazo nazo zimeonesha nia na pia Somalia tunaendelea na mazungumzo.”
Mapema, akitoa maelezo ya ujio wake, Waziri Reshetnikov alisema nchi hizo mbili zimeshakubaliana kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kukuza biashara na uwekezaji na ndiyo maana kesho (Jumanne, Oktoba 29, 2024) watakuwa na kikao cha kwanza cha Tume ya Pamoja ya Kiserikali ya Ushirikiano wa Kiuchumi baina ya Tanzania na Urusi chenye nia ya kuimarisha uhusiano huo. (First Meeting of the Russia-Tanzania Joint Intergovernmental Commission on Trade and Economic Cooperation.)
Alisema kikao hicho ni matokeo ya makubaliano ya kuanzishwa kwa Tume hiyo ya pamoja ambayo yalisainiwa Desemba 29, 2022 ili kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi.
Kwa upande wa elimu, Waziri huyo alisema nchi yake itaendelea kuisaidia Watanzania kunufaika na fursa za masomo nchini Urusi kutokana na bajeti ya Serikali. “Hivi sasa kuna nafasi 90 za wanafunzi wa Kitanzania kusomea vyuo vikuu vya Urusi kuanzia mwaka ujao. Tuko tayari kuongeza idadi hiyo endapo itabidi,” alisema Waziri Reshetnikov.
Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeendelea kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji kwa kujenga barabara, vivuko na madaraja katika maeneo mbalimbali mkoani Katavi ili kuinua shughuli za kijamii na kiuchumi. Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Meneja wa TARURA Mkoa wa Katavi, Mhandisi Japhet Bengesi alisema, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa katika kuimarisha miundombinu ya barabara mkoani Katavi. Mhandisi Japhet amemshukuru Rais Samia kwa kuongeza bajeti ya TARURA mkoa wa Katavi kutoka Shilingi Bilioni 4 hadi kufikia Shilingi Bilioni 15 ambayo…
Mimi ni Binti wa miaka 27, tumejaliwa kupata watoto wawili mimi pamoja na mume wangu, kipindi kabla sijapata hata mtoto mmoja mume wangu alikuwa anawahi kutoka kazini. Tulikuwa tunapendana sana, tulibahatika kupata mtoto mmoj, mume wangu alifurahi sana, tukaa miaka mitatu tukabahatika kupata mtoto wa pili wa kiume . Siku zikaenda, miaka ikapita baada ya hapo mume wangu akawa anachelewa kurudi nyumbani, ukimuuliza anakwambia kazi zilikuwa nyingi na sio kawaida yake kurudi usiku. Akawa anaendelea na tabia, ile ile mwisho wa siku nikimuuliza anakuwa mkali sana na kunigombeza, nikapeleleza kwa majirani zangu wakaniambia mume wako mbona akirudi kazini anapitia kwa…