Nilikuwa nimekaa mbele ya kioo, nikiangalia pua yangu, ngozi yangu yenye madoa na mdomo wangu uliokuwa mwembamba. Sikuwa najipenda. Kilichoniumiza zaidi ni maneno aliyoniambia mtu niliyempenda kwa moyo wangu wote: “Wewe si mrembo, na huwezi kuwa mrembo bila kufanya upasuaji.” Alikuwa mpenzi wangu wa miaka miwili, lakini siku hiyo alikatiza uhusiano wetu kwa kauli hiyo ya kikatili.
Toka utotoni nilikuwa na matatizo ya kujiamini. Nilichekwa sana shuleni, wenzangu waliniita majina kama “kiatu cha mguu mmoja” na “uso wa ndoo.” Nilijua sina ngozi laini kama ya wenzangu, nilikuwa na chunusi za mara kwa mara na nywele zangu hazikuwa laini wala zenye mvuto.
Nilipokuwa mtu mzima, nilijaribu bidhaa nyingi scrubs, serums, hata vipodozi vya bei ghali vilivyosemekana vinatoka Ulaya lakini hakuna kilichobadilika.
Kipindi nilipoingia kwenye uhusiano huo, nilidhani nimempata mtu wa kunikubali jinsi nilivyo. Kwa muda fulani alionyesha kunijali, lakini baadaye alianza kuniambia nivae makeup nene au nijifunge shungi kuficha uso. Mwisho wa yote, akaniambia ukweli wake: siwezi kuwa mrembo kwa hali yangu ya asili. Alinitaka nifanye upasuaji wa sura. Soma zaidi hapa