Hapa duniani kuna njia nyingi za kuweza kufanikiwa kimaisha, changamoto inakuwa jinsi gani utaweza kupata hizo njia na kuzitumia hadi kuweza kufanikiwa.
Kibaya zaidi ni kwamba ni watu wachache sana waliofanikiwa ambao hueleza ukweli kuhusu siri za mafanikio yao, wengi husema uongo kuhofia kupitwa kimafanikio au kukutwa na gundu.
Moja ya njia ambazo zinaonekana kuwa nyepesi kufanikiwa kimaisha ni kubashiri michezo (bet), unapoweka fedha kidogo unaweza kuona utashinda fedha nyingi endapo timu ulizochagua zitashinda kama ulivyobashiri.
Hata hivyo, watu wengi hasa vijana hujikuta katika maisha ya kubet kwa miaka mingi bila kufanikiwa kupata fedha yoyote zaidi ya fedha zao kuzinufaisha kampuni za bet na mawakala wao. Soma zaidi hapa