Kilichotokea siku hiyo siwezi kukisahau. Nilikuwa nimekaa sebuleni nikipanga makabrasha ya mume wangu ambaye pia alikuwa ‘sugar daddy’ wa watu bila mimi kujua. Alikuwa safarini na aliniomba kupitia baadhi ya hati zake kwa ajili ya kukamilisha malipo ya kodi ya mashamba yetu.
Ndipo macho yangu yalipokutana na kitu kilichonifanya nipate kizunguzungu jina la Pamela Mwakipesile kwenye hati halali ya umiliki wa shamba lililokuwa lake kwa zaidi ya miaka saba.
Pamela alikuwa mrembo mdogo sana, mwenye umri wa binti yangu wa kwanza. Nilimjua kwa majina tu kwa sababu ya minong’ono mitaani kuwa ni mmoja wa ‘side chick’ wa mume wangu.
Nilikuwa nikibembeleza nafsi yangu kwamba labda watu walikosea. Lakini sasa, nilikuwa na uthibitisho mkononi: Pamela alikuwa mmiliki wa mali ambayo mimi na mume wangu tuliitafuta kwa jasho letu la miaka mingi. Soma zaidi hapa