Moshi wa mgogoro wa kifamilia ulianza kujitokeza kimyakimya ndani ya nyumba yetu ya ndoa pale nilipoanza kugundua kuwa mume wangu alikuwa akiniona kama mzigo.
Hakuwa tena yule mwanamume niliyeolewa naye kwa upendo; sasa alizungumza kwa kejeli, akinitazama kwa jicho la dharau, na mara nyingi alionyesha wazi kwamba hakuwa na heshima tena kwangu. Sababu? Kwa sababu sikuwa nachangia kipato ndani ya nyumba.
Nilikuwa mama wa nyumbani, nikijitahidi kulea watoto wetu wawili na kuendesha shughuli ndogo ndogo za jikoni. Mume wangu ndiye alikuwa mleta mkate mkuu. Lakini kadiri siku zilivyokwenda, alionekana kuona majukumu hayo kama mzigo unaotoka upande mmoja tu. “Huwezi hata kuchangia mia tano ya umeme?” aliwahi kuniuliza siku moja kwa sauti ya dharau.
Nilijaribu kila njia kujishughulisha. Nilijifunza kutengeneza vitambaa vya meza, nikauza maandazi, hata nikajifunza kupika sabuni. Lakini faida ilikuwa ndogo mno. Na kila niliporudi nyumbani na shilingi elfu moja au mbili, bado alikuwa hathamini. “Pesa ya pipi hii?” alinikejeli mara kadhaa. Nilivunjika moyo. Soma zaidi hapa