Baada ya ukuaji wa teknolojia, bidhaa nyingi na huduma zimekuwa zikitolewa kwa njia ya mtandao, hata hivyo suala hilo limekuwa likiingiliwa na watu wachache ambao sio waaminifu ambao wamekuwa wakitapeli watu fedha zao.
Jambo hilo liliwahi kunitokea kama mwaka mmoja uliopita ambapo nilinunua gari katika mtando mmoja na makubaliano yalikuwa nilipe fedha nusu na nyingine nilipe baada ya kukabidhiwa gari langu.
Basi nililipa fedha zile kupitia akauti ya benki niliyoelekezwa, makubaliano yalikuwa baada ya wiki tatu niletewe gari langu hadi nyumbani lakini haikuwa hivyo.
Kila mara ningewapigia simu na kuwauliza kuhusu hilo na majibu yao yalikuwa kuwa wapo katika mchakato wa kulisafirisha hivyo nisiwe na wasi wasi wowote ule. Soma zaidi hapa