Kwa kweli mapenzi huwa kipimo cha moyo wa binadamu. Nilipokutana na Joel, nilihisi kama ndoto zangu zote kuhusu mwanaume wa ndoto zangu zimefikia ukingoni. Alikuwa mpole, mchangamfu, mkarimu na mwenye ndoto za maisha. Aliniahidi kunioa, alinijumuisha kwa familia yake, na hata alijenga mazingira ya kuonyesha kuwa uhusiano wetu ulikuwa wa kudumu.
Kwa miaka miwili, nilimhudumia kama mke halali. Nilikuwa nikimpikia, kumfulia, hata kusaidia kwenye biashara zake za mtandaoni. Kila alipopata hela, aliniahidi kuninunulia pete ya uchumba na kunipeleka kumtambulisha kwa wazazi wake rasmi. Lakini siku zilikuwa zinapita bila hatua yoyote.
Kilichonitia wasiwasi zaidi ni ndoto za ajabu nilizokuwa nikianza kuota. Mara naota nipo kwenye makaburi nikitawazwa, mara naota nimevaa mavazi ya harusi huku watu wote wamevaa nguo nyeusi za maombolezo. Mwili wangu pia ulianza kuchoka kila mara, usingizi wa mara kwa mara, na kupoteza nguvu ya kuamka asubuhi.
Mara kwa mara nilihisi kama kuna kitu kisicho cha kawaida kinachoendelea. Nilipojaribu kumkabili Joel kuhusu ahadi ya ndoa, alianza kunikasirikia ghafla. Akawa na hasira zisizoeleweka, akaanza kunikwepa, na hata kunitusi. Marafiki zangu walianza kunionya kuwa kuna kitu cha ajabu kuhusu Joel. Baadhi yao walidai kuwa walimsikia akijigamba kuwa amefanikiwa kisiri kwa kutumia “nguvu ya mwanamke mjinga” ambaye hajui anatumikishwa. Soma zaidi hapa