Kwa hakika mimi ni miongoni mwa vijana waliochelewa sana kuoa, ilifikia hatua hadi kwenye familia waliniambia wanitafute mwanamke lakini nilikataa kwa kuona aibu.
Changato yangu kubwa ilikuwa ni kwamba kila nikipata mwanamke sidumu naye kabisa, tukikaa pamoja miezi kadhaa na kuanza kupanga mipango ya maisha ya mbeleni, basi ghafla linatokea jambo la kutuachanisha.
Jambo hili lilikuwa linaniumiza sana kwa sababu nilikuwa najimudu kabisa kimaisha, nilikuwa na uwezo wa kumgharamikia mwanamke kila kitu lakini nashangaa kwanini hawataki kudumu na mimi.
Nilikuwa naona aibu kila mara kuhudhuria harusi za wenzangu lakini ukija upande wangu sina hata mchumba wa kupanga naye hiyo mipango ya harusi. Soma zaidi hapa