Wakazi wa kijiji cha Kinyamaseke kilichopo mkoani Kigoma, Jumatatu, Agosti 4, 2025, walipata taswira ya nadra sana kushuhudiwa katika maisha ya kawaida, baada ya tukio la kushangaza kuwafanya watu kusimama barabarani, wengine wakipiga video na wengine wakishindwa hata kuamini macho yao.
Kisa kilianza mapema asubuhi baada ya wanakijiji kuona mzinga wa nyuki ukishuka kutoka mti mkubwa uliokuwa pembezoni mwa barabara na kuzunguka wanaume wawili waliokuwa wakitembea kwa haraka huku wakiwa na mabegi makubwa yenye uzito usio wa kawaida.
Kwa mujibu wa mashuhuda, wanaume hao walijaribu mara kadhaa kupiga hatua za haraka ili kuondoka, lakini nyuki hao walionekana kama wamepewa mafunzo ya ulinzi, kwani walizunguka miili ya watuhumiwa kwa mpangilio wa ajabu, wakizungusha miduara kana kwamba ni askari waliowaziba njia. Soma zaidi hapa