Mtaa wa mjini uligeuka uwanja wa mshangao baada ya mwanamke mmoja kuonekana akikimbia barabarani akiwa na mavazi ya ndani tu huku akipiga mayowe ya kuomba msaada, hali iliyowashangaza wakazi waliokuwa karibu na eneo hilo, hasa baada ya kubainika kuwa alikuwa ameingia chumba cha kulala na mume wa mtu.
Kwa mujibu wa walioshuhudia tukio hilo, kilio cha mwanamke huyo kilianza majira ya saa mbili na nusu asubuhi kutoka katika moja ya nyumba za kulala wageni, ambako watu walieleza kuwa mwanamke huyo aliingia pamoja na mwanaume aliyedaiwa kuwa fundi maarufu wa umeme mtaani hapo, ambaye alifahamika kwa jina moja tu la Mwagito.
Waliosikia mayowe hayo walidhani mwanamke huyo alikuwa amepigwa ama kuna jaribio la uhalifu, lakini walipojaribu kukaribia eneo la tukio, walishangazwa kuona nyuki wamejaa hewani, wakizunguka lango la nyumba hiyo na sehemu ya paa, huku wengine wakiwa wameingia chumbani walikoelekea wapendanao hao. Soma zaidi hapa