Kilichotarajiwa kuwa mchana wa furaha kiligeuka kuwa tafrani ya kushangaza mjini Dodoma siku ya Jumatano, Agosti 6, 2025, baada ya mwanadada mmoja kujikuta akipagawa ghafla mbele ya wachumba watatu aliokuwa amewadanganya kwa miezi tofauti, tukio lililozua kioja na sintofahamu kubwa mbele ya watu waliokuwa wakihudhuria hafla ya kipaimara ya mtoto wa jirani.
Watu walianza kumshangaa msichana huyo, aitwaye Doreen, baada ya kuonekana akiwa amevalia mavazi ya kuvutia, akizunguka eneo hilo akionekana mwenye furaha kupita kiasi, kabla ya hali kubadilika ghafla na kuanza kupiga kelele akisema anahisi “mioyo mitatu ikimpasuka kwa wakati mmoja,” jambo lililowafanya watu waanze kumuangalia kwa hofu.
Kabla ya watu kuelewa kilichokuwa kinaendelea, vijana watatu tofauti waliokuwa miongoni mwa wageni waalikwa walitambua kuwa wote walikuwa wakiwasiliana kimapenzi na Doreen kwa wakati mmoja, kila mmoja akidhani ndiye mchumba halali, huku kila mmoja akiwa na picha za pamoja naye kwenye simu zao. Soma zaidi hapa