Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Beno Malisa Agosti 22, 2025 amemkabidhi boti moja mpya PB.44 ULINZI Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga. Akikabidhi boti hiyo kwa Jeshi Mkoa wa Mbeya, Mhe Malisa amelitaka Jeshi hilo kulitumia vizuri boti hilo katika kuimarisha doria za ziwa nyasa Wilayani Kyela na kutokomeza uhalifu. nipe vichwa vitano vya habari Aidha, Mhe.Malisa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura kwa kutimiza ahadi ya kutoa boti kwa ajili ya kuimarisha ulinzi Ziwa Nyasa na kuahidi kuitunza na kuitumia vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa. Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga amesema kuwa Boti hiyo inakwenda kuimarisha ulinzi Ziwa Nyasa kupitia doria za pamoja za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, JWTZ, Uhamiaji na TRA. Ziwa nyasa ni miongoni mwa maziwa makuu nchini ambalo sehemu ya Ziwa hilo ni nchi jirani ya Malawi na Mkoa wa Njombe na Ruvuma hivyo uwepo wa Boti hiyo ni mikakati ya kuimarisha ulinzi na kudhibiti uhalifu wa majini.
Trending
- Niliwahi Kudharauliwa Kwa Kutokuwa na Mali Lakini Sasa Nimegeuka Mfano wa Mafanikio
- RC Mbeya Akabidhi Boti Mpya ya Ulinzi Jeshi la Polisi kwa Doria Ziwa Nyasa
- BENKI YA NMB YAWACHIA FURAHA WAGONJWA HOSPITALI YA RUFAA MKOA MBEYA YAKABIDHI VITANDA 20 NA MAGODORO
- Njia Sahihi za Kujilinda Dhidi ya Uchawi na Roho za Wivu
- Jamaa Akimbia Harusi Yake Mwenyewe Akisema Anahisi Kuvutwa Na Upendo Wa Ex Wake
- Wafanyabiashara wadogo wapata utulivu wa kimaisha kupitia msaada wa pekee
- “Polisi Mbeya Wamnasa Mwindaji Haramu na Meno ya Tembo”
- “Mwanamke Mbeya Akamatwa na Vifaa vya Umeme TANESCO Nyumbani Kwake”