Diwani wa Kata ya Ilomba, Ndg. Noah Edson Mwakisu, leo amerejesha fomu za kuwania Umeya wa Jiji la Mbeya kupitia CCM. Akizungumza katika Ofisi za CCM Mbeya Mjini, Mwakisu alisema anagombea nafasi hiyo ili kulipa jiji mwelekeo mpya wa maendeleo, akisisitiza umuhimu wa uongozi wenye maono, ushirikiano na uwajibikaji.
Mwakisu alisema Mbeya ina fursa kubwa za kimaendeleo kutokana na mazingira na jiografia yake, hivyo inahitaji kiongozi anayeendana na mahitaji ya kizazi cha sasa, hususan vijana ambao ndio nguvu ya uchumi wa jiji. Aliomba sapoti na baraka za wananchi, akiahidi kulifanya jiji hilo mfano wa kuigwa endapo atapewa dhamana.
Kurejesha fomu hizo kunamweka rasmi katika kinyang’anyiro cha ndani ya CCM cha kuwania Umeya wa Jiji la Mbeya mwaka huu.
Trending
- Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Aga Khan Zaanzisha Ushirikiano wa Kuboresha Huduma za Afya
- Shule ya Sekondari Utengule Usangu, H
- Mradi wa Barabara Mlima Nyoka Wamfikisha MCC ASAS, Ataka Kero za Wananchi Zitokomee
- Mradi wa Soko la Matola Wakwama, Meya na MNEC Wakanusha Kukamilika Mei
- JK KWA MFALME MSWATI III KUJADILI UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA KWA NCHI WANACHAMA WA ECSA
- Halmashauri Yaipongeza Mbeya UWSA Kwa Mradi wa Maji, Asema Utakuza Uwekezaji
- Mpango wa Maendeleo 2026/27: Kasaka Apongeza Mafanikio, Aomba Maboresho
- Msafara Wasimama Soweto, Mbunge Mwalunenge Aamuru TANROADS Kuondoa Dimbwi la Miaka 3 Mara Moja

