Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kwa namna moja au nyingine kuna baadhi ya taasisi za dini zimejiingiza kwenye mkumbo ambao unaendelea wenye nia ovu ndani yake. Akieleza juu ya uongozi wa nchi katika kufuata misingi ya katiba na sheria, Rais Dkt. Samia amesema Tanzania haina dini lakini Watanzania wana dini za madhehebu mbalimbali huku akisisitiza kuwa kikatiba na sheria za nchi hakuna dini na dhehebu lolote lenye uwezo wa’kuover ride’ madhehebu mengine. Akizungumza na Wazee wa mkoa wa Dar es salaam leo tarehe 2 Disemba 2025, Rais DKt. Samia ameyasema na kuyasisitizia haya kuhusu taasisi za dini nchini “Viongozi wa dini msijivishe majoho ya kwamba nyinyi ndio mnaweza ‘kuover run’ nchi hii, hakuna. Tutakwenda kwa kwa Katiba na Sheria ya Nchi hii.” “Hatutaendeshwa na madhehebu yoyote ya dini, madhehebu ya dini na wafuasi wao” “ubora wa dini upo miyoyoni kwetu, wale wanaoamini ndio wanajua ubora wa dini yao..” “hakuna ‘over riding’ hapa! Kwamba “mimi dini yangu ndio itaover ride Tanzania na tamko nikilitoa ndio hilo hilo”. “…hata wenyewe wanatofautiana, mimi toka nimekaa matamko 8 yametolewa na TEC, lakini ukienda chini chini wenyewe wanapingana, matamko yale hayafanyi kazi…waliosimama kwenye mstari wa haki wanaona ni batili iliyofanyika..hawaungani nao..” “Tanzania yetu ni nchi ya umoja na mshikamano, amani na utulivu ndio ngazo zetu, tusivurugwe ndugu zangu
Trending
- Hakukata tamaa hadi alipopata mtoto wake kwa njia hii
- SAMIA: VIONGOZI WA DINI MSIJIVISHE MAJOHO KUONGOZA NCHI – AWANYOOSHEA KIDOLE TEC
- Yard yake ilianza kujaza wateja kutoka pande zote
- RAIS SAMIA AFUNGUKA MAZITO MBELE YA WAZEE!
- Mkutano mkuu Simba vurugu tupu
- KANISA LA EAGT BETHELI GOMBE UYOLE MBEYA NA UJUMBE MZITO KATIKA KUCHANGIA UJENZI WA KANISA LAO
- DKT TULIA HAPOI WALA HABOI AENDELEA KUSAMBAZA UPENDO KWA WAPIGA KURA WAKE KATA YA ILEMI.*
- Suluhisho kwa wanawake wanaokuwa wakavu wakati wa tendo la ndoa

