Author: Mbeya Yetu

#MbeyaYetuTv
Mfanyabiashara mkubwa wa Madini aina ya dhahabu wilayani Chunya mkoani Mbeya amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya pamoja na wafanyabiashara wenzie wanne wakikabiliwa na kosa la uhujumu wa Uchumi, Kutakatisha fedha, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kupatikana na Madini aina ya Dhahabu kinyume cha sheria,.

Read More

#MbeyaYetuTv
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi Sugu ameachana na ukapera na kuamua kufunga pingu ya Maisha na Mchumba wake Happiness Msonga.Ibada ya Ndoa ya Sugu imefanyika katika Kanisa Katoliki la Ruanda Jijini Mbeya.Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Freeman Mbowe,wabunge Joseph Selasini, Wilfred Lwakatare na MwanaHip Hop mwenzie Mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu Profesa Jay waliungana naye katika sherehe hiyo.

Read More

#MbeyaYetuTv
Sakata la watuhumiwa wa mauaji ya mkazi wa Chunya Tenson Ndege Meta,kudaiwa kuachiwa huru, limechukua sura mpya baada ya Kaimu Mkuu wa Mashtaka mkoa wa Mbeya Basilius Namkambe kutoa msimamo wake na kuelezea namna taarifa zilizomo kwenye jalada la Daktari zinavyotofautiana na taarifa zinazodaiwa kuelezwa na ndugu wa marehemu,
Wakili Msomi Namkambe amesema kuwa anashangazwa na taarifa zinazodaiwa na wanandugu kufukuzwa wakati wa kufanyiwa uchunguzi mwili wa marehemu ilhali katika taarifa iliyowasilishwa na Daktari aliyefanya uchunguzi zimemuandika mmoja wa mashuhuda kuwa ni mke wa marehemu Rehema Daimon.l

Read More