Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- MTARO ULIOFUKIWA MTAA WA LUMBILA IWAMBI MBEYA WAFURIKA MAJI YA MVUA NA KUIBUA KIZAAZAA KWA WANANCHI
- Mauzo yalianza kuongezeka, wateja wakawa wakudumu!
- Mtoto wa Jenista Mhagama Aibua Hisia Kali, Asema Mama Yake Hana Deni
- RAIS SAMIA KWA UCHUNGU MSIBANI – ”TUTALIMISI TABASAMU LAKE –
- MADEREVA BODABODA MKOANI IRINGA WALAANI VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI.
- MAHAFALI YA 23 YA TAASISI YA UHASIBU TIA KAMPASI YA MBEYA, RC MALISA AWAALIKA WAWEKEZAJI MKOANI MBEYA.
- Ilinde biashara dhidi ya husda na mikosi
- Fanya hivi kuvutia fursa mpya za kazi
Author: Mbeya Yetu
Mbeya, Agosti 2025 – Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mbeya imetangaza kufanikisha uokoaji wa zaidi ya shilingi milioni 47 na kuziwezesha Halmashauri kuongeza mapato ya ndani kwa zaidi ya shilingi milioni 200 kupitia ufuatiliaji na udhibiti wa mianya ya rushwa na upotevu wa fedha za umma. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya, Maghela P. Ndimbo, mafanikio hayo yametokana na kazi za ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, uchambuzi wa mifumo ya ukusanyaji mapato, na kudhibiti matumizi yasiyo sahihi ya fedha katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2025. Miradi ya Maendeleo…
*Katibu Wa Siasa na Wenezi Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbeya Mjini Ndugu, Philimon Mng’ong’o Chatangaza Majina ya Madiwani Wateule Jimbo la Mbeya Mjini*
*#Oktoba Tunatiki*
*#Kazi na Utu Tunasonga Mbele*
*Katibu Wa Siasa na Wenezi Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbeya Mjini Ndugu, Philimon Mng’ong’o Atangaza Majina ya Madiwani Wateule Jimbo la Uyole*
*#Oktoba Tunatiki*
*#Kazi na Utu Tunasonga Mbele*
GOAL 3 Yakabidhi Monitors 15 za Kisasa Hospitali ya Rufaa Mbeya Yaimarisha Huduma za Watoto Wachanga
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imepokea vifaa tiba vya kisasa monitor 15 kwa lengo la kuboresha huduma za uangalizi kwa watoto wachanga. Vifaa hivi, vilivyotolewa na Madau wa Maendeleo GOAL 3, vinatarajiwa kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya kwa watoto wanaohitaji msaada wa haraka na wa kitaalamu.
Akikabidhi vifaa tiba hivyo Mwamvuwa Mika Meneja Mradi Tanzania amesema thamira ya Goal 3 ni hakikisha Watoto wachanga wananzaliwa katika mazingira mazuri na pia wanapata huduma ambayo ni bora.
“Kwa kipindi hiki tumefika hapa hospitali ya rufaa ya kanda Mbeya kwaajili ya kufunga Impala monitors kwenye kitengo cha NIKU ili kuweza kuwasaidia Watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya muda. Ningependa pia kutoa shukrani zangu za dhati kwa Uongozi wa hospitali kwasababu tumeweza kushirikiana hadi kwa hatua hii tuliofika leo ambapo tumeshazifunga monitors 15 na zimeshaanza kutoa huduma kwa Watoto walio wodini na pia tutaendelea kushirikiana ili kuwafika Watoto wengine walio kwenye hospitali zingine ” – Mwamvuwa
Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Bi. Myriam Msalale amemshukuru Madau wa maendeleo GOAL 3 kwa kuichagua Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kufanya kazi nayo na kuvipatia vifaa tiba hivyo ambavyo vimekuja kwa wakati na vitatusaidia sana katika kuboresha huduma kwa watoto wachanga na kutoa wito kwa watumiaji wa vifaa tiba hivyo kuvitunza kwa uangalifu wa hali ya juu ili viweze kudumu kwa muda mrefu na kuwahudumia Watoto waliokuja kupata matibabu.
.
Nae Dkt.Rehema Marando Daktari Bingwa mbobezi wa watoto wachanga, amesema kuwa msaada huo umeleta manufaa makubwa kwa watoa huduma na Watoto ambapo vitawezesha kuboresha huduma na kuongeza ufanisi wa utoaji wa matibabu na uangalizi wa hali ya juu kwa Watoto wachanga.
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha National Convention for Construction and Reform – Mageuzi (NCCR-MAGEUZI), Mhe. Haji Ambar Khamis akiwa na Mgombea Mwenza, Mhe. Dkt. Eveline Wilbard Munisi wakionesha begi la fomu za uteuzi baada ya kukabidhiwa na Tume leo Agosti 15,2025. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha National Convention for Construction…
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT – Wazalendo), Mhe. Luhaga Joelson Mpina. Alichukua fomu hizo leo Agosti 15, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. (Picha na INEC). Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa…
