Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI
- KWA MARA NYINGINE, MHANDISI MAHUNDI AWAPA NEEMA WAGONJWA WA MACHO
- MWAKIPESILE AREJESHA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI
- Msimu wa pili wa tamasha la michezo na vipaji MZRH
- MKULIMA NA MFUGAJI WA MBARALI ATIA TIMU KIPUTE JIMBO LA MBARALI USANGU ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE
- WAKILI MSOMI KAPTENI MSTAAFU SAMBWEE SHITAMBALA ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI.
- MWAISUMBE: ALIYEJITOSA UBUNGE 2010 AWANIA TENA MBEYA MJINI AAHIDI KUMUUNGA MKONO ATAKAYETEULIWA
- MHASIBU SUA AJITOSA UBUNGE JIMBO LA SAME MASHARIKI
Author: Mbeya Yetu
*MBUNGE MASACHE AUNGURUMA NKUNG’UNGU*
Lupa 📍
Mbunge wa lupa-chunya *Mh Masache Kasaka* ameambatana na *Mh Juma Homera* mkuu wa mkoa wa mbeya katika ziara ya wilaya ya chunya lengo kubwa ni kusikikiliza kero za wananchi wa katika kata na vitongoji mbali mbali na kuzitafutia ufumbuzi.
Katika ziara hiyo *Mh Masache kasaka* amezungumza na wananchi hao na kupokea kero zao ikiwemo barabara itokayo mwanzo mgumu kuunganisha ngwala itafikishwa kwa *Mh Samia Suluhu* ili iweze kupatiwa ufumbuzi.
Sambamba na hilo *Mh Masache kasaka* ameshukuru serikali inayoongozwa na Rais *Mh Dkt Samia Suluhu* kwa namna alivyoweza kutekeleza miradi mbali mbali katika kata hiyo ya nkung’ungu na kuweka mabadiriko ambayo awali hayakuwepo.
*KAZI NA UTU*
*CHUNYA TUNASONGA MBELE*
*DKT. TULIA ATANGAZA KUGOMBEA JIMBO LA UYOLE*
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ametangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo jipya la Uyole mkoani Mbeya katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Dkt. Tulia ametoa tamko hilo leo tarehe 23 Mei, 2025 alipokuwa akihutubia Mkutano Mkuu Maalum wa Wilaya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo amesema kuwa ameamua kufanya uamuzi huo ili kuwahudumia wananchi wa Uyole kutokana na kasi ndogo ya maendeleo iliyopo katika eneo hilo.
“Maendeleo ya Uyole yanasonga kwa taratibu sana, nimeona ni vyema nijitoe kwa moyo wote kuhakikisha wananchi wa Uyole wanapata huduma stahiki na maendeleo ya haraka. Nitoe wito kwenu, watu wengi watakuja kwenu, chagueni kiongozi, chagueni mtumishi, itasaidia sana kuendelea kuyakimbiza maendeleo ya jamii,” amesema Dkt. Tulia.
TUNAMTAKA DKT TULIA AGOMBEE UYOLE SABABU YA MAENDELEO.
Wananchi wa maeneo mbalimbali katika Jimbo jipya la uyole wamemtaka mbunge wa Mbeya Mjini Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Mabunge duniani Dkt Tulia Akson kugombea jimbo la Uyole sababu ya utendaji mzuri wa kazi na kuleta maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumhiya ya vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM wilaya ya Mbeya mjini Ameishukuru Tume ya uchaguzi kwa kuligawa jimbo hilo akieleza yakuwa kutakuwa na maendeleo ya Kasi katika Maeneo mbalimbali.
Watoa huduma ya Afya ya Mama na mtoto wametakiwa kuwa makini wakati wa utoaji huduma ya uzazi ili mama anapokuwa analeta zawadi ya mtoto duniani hasibaki na changamoto yoyote ya kiafya ikiwemo ugonjwa wa fistula. Leo Mei 21,2025 Wizara ya Afya Idara ya Mama na Mtoto inakaa Jijini Mbeya pamoja na Wadau kujadili afua muhimu za kuangazia namna bora ya kupambana na ugonjwa wa Fistula kwa akina mama kuelekea maadhimisho ya siku ya Fistula Duniani itakaoyadhimishwa Kitaifa Mbeya Mei 23, 2025. Mkurugenzi Hospitali ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekilage wakati…
Na Mwandishi `Maalumu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa maono yake ya mbali na uamuzi wa busara wa kumpendekeza Profesa Mohamed Yakub Janabi kugombea nafasi ya Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Wananchi mbalimbali waliohojiwa wametaja hatua hiyo ya Rais Samia kama ishara ya kujiamini kama taifa, na uthibitisho kuwa Watanzania wanao uwezo wa kushika nafasi nyeti katika taasisi kubwa za kimataifa, wakielezea faraja yao kwa jinsi Tanzania inavyozidi kung’ara kwenye majukwaa ya kidiplomasia duniani. Aidha, Rais Samia amesifiwa kwa kuunda kikosi kazi maalum kilichoongozwa na Rais…