Browsing: Video Mpya

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 2 Machi, 2024 ameshiriki katika Jopo la kujadili “Jukumu la Mabunge katika kuendeleza amani na maendeleo Duniani” ambalo ni sehemu ya Mkutano wa Kidiplomasia wa Antalya ulioanza jana tarehe 1 Machi 2024 kwa kufunguliwa na Mhe. Recep Tayyip Erdogan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki.

Dkt. Tulia aliongoza sehemu ya majadiliano hayo na kuelezea namna Bunge linavyoendelea kuchagiza amani na demokrasia nchini Tanzania pamoja na Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unavyoendelea kutafuta suluhu na amani kwa Wanachama wake wakiwamo Urusi na Ukraine, Israel na Palestina, Azerbaijan na Armenia na wengine ambao wapo katika migogoro ya kukosa amani.

Mkutano huu unatarajiwa kuhitimishwa kesho tarehe 3 Machi, 2024 Jijini Antalya, Uturuki.

Maadhimisho ya siku ya usikivu Duniani yameadhimishwa Kitaifa Mkoani Mbeya mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aliyewakilishwa na Dkt Maisara Karume maadhimisho yalifofanyika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Katika hotuba yake Dkt Maisara Karume amesema takwimu za kitaifa zinaonesha kuwa tatizo la usikivu ni kubwa na baadhi ya mikoa wanawake wanaongoza kwa tatizo la usikivu.

Dkt Maisara ameagiza hospitali zote za Rufaa za mikoa nchini kuwa na vifaa kwa ajili kubaini changamoto ya usikivu kwa wananchi.

Rais wa Jumuia ya Wataalamu wa masikio,pua na koo Tanzania Dkt Edwin Liyombo ameishukuru serikali kwa kuongeza wataalamu na vifaa katika hospitali nyingi nchini.

Naye Amina Mfaki mwakilishi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI amesema serikali inaendelea kuboresha huduma za afya kwa kujenga hospitali sanjari na kutoa elimu kwenye jamili ili kupunguza tatizo la usikivu kwa wananchi.

Taarifa imesomwa na Raphael Gabriel Katibu wa Jumuia ya wataalamu wa masikio pua na koo ikionesha Jumuia ina wataalamu zaidi ya mia moja ishirini wa kada mbalimbsli ambao walihusika kutoa huduma za afya,uchunguzi na utabibu katika wiki ya maadhimisho.

Dkt Benedict Ngunyale ni Daktari Bingwa hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya mkuu wa kiitengo cha masikio,pua na koo amesema katika wiki ya maadhimisho wamezifikia shule kumi na moja za msingi na zaidi ya wanafunzi elfu tatu wamepatiwa elimu na uchunguzi wa masikio na matibabu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya Dkt
Godlove Mbwanji amesema changamoto nyingi za usikivu zinasababishwa na upigaji wa muziki kwa sauti ya juu mathalani kwenye huduma za vinyozi ambazo huathiri pia wateja.

Mwinyi Kondo kutoka Wizara ya Afya ameomba vyombo vya habari kutoa nafasi kwa waataalamu kutoa elimu kwenye jamii.

Kupitia maadhimisho haya mbali ya wananchi kunufaika na elimu kutoka kwa wataalamu wa wananchi wamefanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu bure.

Jumuia ya watumia maji ngazi 60 wamejitokeza kupanda miti zaidi ya 2000 chanzo cha Nzovwe 2 lengo kwa mwaka huu ni kupanda miti 10000 ili kutunza vyanzo mbalimbali Jijini Mbeya.

Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Vulustan David amesema zoezi hilo ni endelevu.

Kwa upande wake Mratibu wa Jumuia ya watumia maji bonde la Ziwa Rukwa Rhoda Mwinuka amewataka wananchi waofanya shughuli za kibinadamu ambazo ni pamoja na kilimo kuacha mara moja kabla hawajachuliwa hatua za kisheria.

Mwenyekiti wa mtaa wa Bomba mbili Kata ya Mwakibete amesema mpsngo huo ni endelevu ili kutunza vyanzo vya maji.