Browsing: Video Mpya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera ameagiza kukamatwa na kichunguzwa viongozi wa chama kikuu cha ushirika wilayani Kyela (KYECU) Kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kupelekea upotevu wa zaidi ya millioni 440 za wakulima, baada ya magunia zaidi ya 200 kutoonekana baada ya mnada namba tatu wa zao la cocoa uliofanyika jumatatu July 15 wilayani humo.

Pamoja na kukamatwa viongozi hao akiwemo mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wilayani Kyela (KYECU) Evance Mwaipopo pamoja na Meneja wa chama hicho Julius Mwankenja, Homera ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Mbeya, kuchunguza chama hicho mifumo yao ya kifedha huku akisitisha taratibu zote za manunuzi Hadi pale kamati ya ulinzi na usalama itakapo jiridhiaha.

Awali akiwasilisha taarifa Kwa mkuu wa Mkoa, mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe Josephine Manasi, amesema hasara hiyo imeonekana baada ya mnunuzi aliyeshinda mnada namba tatu kubaini magunia zaidi ya 200 hayopo kwenye maghara kati ya magunia 1,915 yaliyoshindanishwa kwenye mnada huo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamini Kuzaga kumsaka na kumkamata Kijana anayepatikana Ntokela Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya Kwa Kosa la Kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Maneno Makali na Kisha kuichoma moto Picha inayomuonyesha Mh:Rais.

RC Homera amelaani vikali Kitendo hicho kuwa si Cha Maadili Wala Uungwana na Kiko tofauti na Utamaduni halisi wa Wananchi Mkoani Mbeya.

Hata hivyo ametoa Masaa 24 kwa Kamanda Kuzaga Kumkamata Kijana huyo ili alisaidie Jeshi la Polisi juu ya tuhuma hizo na Mashambulizi hayo ambayo kayaelekeza Moja kwa Moja kwa Mh: Rais Dkt: Samia Suluhu Hassan.

Mwisho RC Homera amewasihi Wananchi Mkoani Mbeya kutojiingiza kwenye Vitendo viovu kwa Kukashifu Viongozi Makusudi badala yake wajikite katika Utafutaji na Uchapa Kazi kwa Manufaa ya Familia zao na Tanzania kwa Ujumla.

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 24 Mei 2024, ametembelea Kanisa la Mtakatifu Bikira Maria lililopo Cairo nchini Misri, eneo ambalo Bikira Maria alijificha na Mtoto Yesu kufuatia tishio la Mfalme Herode kutaka kumuua Mtoto Yesu. Ziara hii inasisitiza umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuendeleza amani, umoja na kuwa na uelewa wa pamoja katika imani na utamaduni wetu.