Browsing: Video Mpya

CPA. Gilbert Kayange, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya leo tarehe 16/11/2024 ametembea mtaa kwa mtaa kusikiliza na kutatua changamoto za wateja pamoja na kukagua miradi inayotekelezwa na Mamlaka.

Mkurugenzi Mtendaji ametembelea na kukagua mradi wa maji wa mto Simba, mradi wa kuboresha huduma ya maji kupitia visima virefu vya Gombe kusini na Mwasenkwa na mradi wa kuboresha huduma ya maji katika Kata ya Iyunga.

CPA. Kayange amesema, Serikali inawekeza fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya kuboresha huduma ya maji katika Jiji la Mbeya na Mji wa Mbalizi ili kuhakikisha kwamba Wananchi wanapata huduma bora na endelevu .

Aidha, katika ziara hiyo CPA. Kayange ameshuhudia miradi ambayo imefika hatua ya kuanza kuhudumia na kunufaisha wakazi wa maeneo mbalimbali. Mradi hiyo ni mradi wa kuboresha upatikani wa huduma ya maji Gombe Kusini na mradi wa mto Simba ambao unanufaisha Wananchi wa maeneo ya Mwasanga, Tembela, Ijombee na Sitoi.

Vile vile, Mkurugenzi Mtendaji amewaasa Wananchi kutoharibu miundombinu ya maji kwa kujifanyia maunganisho yasiyo halali na kuisababishia Taasisi hasara kupitia upotevu wa maji na kuathiri upatikanaji wa huduma ya majisafi kwa wananchi wengine.

Aidha, CPA. Kayange ametoa wito kwa Wananchi kulipa ankara za maji kwa wakati ili kuijengea Mamlaka uwezo wa kutoa huduma endelevu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 16 Novemba, 2024 amefungua Mkutano wa Kibunge wakati wa Mkutano wa 29 wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Jijini Baku Azerbaijan.

Mkutano huo uliohudhuriwa na Wabunge zaidi ya 300, umejadili njia mbalimbali zinazojumuisha majukumu halisi ya Kibunge katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi na athari zake na namna bora ya kuzisaidia nchi zinazoathirika zaidi na mabadiliko hayo hususani nchi za visiwa vidogo.

Majadiliano hayo ya siku mbili yanatarajiwa kuhitimishwa kesho tarehe 17 ambapo Umoja wa Mabunge utatoa maazimio yatayotarajiwa kufikiwa kwa pamoja kwenye Mkutano huo.

Mbeya. Watu 11 wamefariki dunia na wengine 20 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea leo Septemba 27 wilayani Mbeya mkoani hapa.

Ajali hiyo imetokea eneo la Jojo Kata ya Ilembo wilayani humo ikihusisha gari aina ya Fuso ambayo ilikiwa ikielekea kwenye soko kwa ajili ya mnada.

Mmoja wa mashuhuda katika eneo hilo, Elias Shiwiwi amesema gari hilo kampuni ya Chakazi likiwa limebeba wafanyabiashara kwa ajili ya mnada wa leo, lilikatika propela na kusababisha vifo kadhaa.

“Palepale wamefariki watano, baadaye wengine watano wakafia njiani wakielekea kituo cha afya Ilembo nikiwa naona hadi kufika kituoni hapo” amesema Shiwiwi.

Mganga mkuu wa kituo cha Afya Ilembo, Dk Philimon Irungi amethibitisha kupokea miili ya watu 11 ambapo mwingine mmoja alifariki baada ya kufika kituoni hapo.

“Eneo la tukio walifariki 11, ikatangulia miili sita kisha ikaja mitano na mmoja akafariki wakati akipatiwa matibabu, majeruhi ni 21” amesema Dk Urungi.