Author: admin

*“SERIKALI IRUHUSU MAGARI YA ABIRIA KUSAFIRI WAKATI WOTE HADI USIKU”- DKT. TULIA*

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameitaka Serikali kuangalia upya utaratibu uliowekwa katika baadhi ya maeneo nchini wa kuyazuia magari ya abiria kufanya shughuli za usafirishaji nyakati za usiku kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya kiuchumi.

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo Novemba 10, 2022 wakati aliposhiriki Semina kwa Wabunge kuhusu usalama Barabarani iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

Amesema kuwa ni lazima ifike wakati sasa Wananchi waweze kufanya shughuli zao muda wote na kuondoa dhana iliyozoeleka ya magari ya abiria kuwekewa vikwazo vya kufanya kazi kwa sababu zizisokuwa rasmi wakati magari mengine yakiwemo ya mizigo yanaruhusiwa.

“Kunashida gani ya kuzuia gari ya abiria kusafiri usiku? Tunatamani nchi yetu kuchangamka Zaidi kiuchumi sasa kwanini magari haya yawe na zuio wakati magari mengine yanaruhusiwa kusafiri hadi usiku. Kama ni changamoto ya miundombinu basi ishughulikiwe na shughuli zifanyike” amesisitiza Dkt. Tulia

Read More

AJALI YA GARI KUGONGA MAGARI MATATU NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI.Ni kwamba mnamo tarehe 16.08.2022 majira ya saa 02:00 asubuhi huko maeneo ya Inyala Pipeline, Kijiji cha Shamwengo, Kata ya Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya – Njombe, Gari lori lenye namba za usajili T.387 DFJ lenye tela namba T.918 DFE aina ya Dayun likiendeshwa na Dereva MUHSIN GUMBO, Mkazi wa Dar es Salaam mali ya kampuni ya Evarest Frech Ltd likiwa na kontena la mchanga likitokea Mbeya liligonga kwa nyuma Gari T.966 DUQ aina ya Fuso basi mali ya kampuni ya Super Rojas likitokea Mbeya kuelekea Njombe likiendeshwa na ALEX MGIMBA [51] Mkazi wa Jijini Mbeya na kisha kugonga Gari T.836 DRE Mitsubish Benz iliyokuwa ikiendeshwa na NEDIM PREMJI, Mkazi wa Dar es Salaam na kisha kugonga Gari linguine T.342 CHG/T.989 CGS Scania iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika na kusababisha vifo vya watu 19 kati yao wanaume ni 12, wanawake 06 na mtoto 01. Aidha katika ajali hiyo majeruhi ni 10 kati yao wanaume ni 07, wanawake ni 02 na mtoto 01.Chanzo cha ajali ni Gari kufeli breki kwenye eneo lenye mteremko mkali na kisha kugonga magari mengine. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na Hospitali ya Igawilo. Imetolewa na:Ulrich Matei – SACPKamanda wa Polisi,Mkoa wa Mbeya.

Read More