Browsing: Video Mpya

#mbeyayetutv
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 26 Julai, 2024 amemkabidhi nyumba ya kuishi Mzee Ambalile Mwala ambaye amekuwa akiishi katika mazingira magumu pamoja na familia yake katika Kata ya Ching’anda Mlimba Mkoani Morogoro. Nyumba hiyo imejengwa na taasisi ya Tulia Trust.

Pamoja na hayo, Dkt. Tulia ametoa msaada wa madaftari, kiti mwendo kwa wahitaji na malumalu kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Kata ya Ching’anda Halmashauri ya Mlimba Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera ameagiza kukamatwa na kichunguzwa viongozi wa chama kikuu cha ushirika wilayani Kyela (KYECU) Kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kupelekea upotevu wa zaidi ya millioni 440 za wakulima, baada ya magunia zaidi ya 200 kutoonekana baada ya mnada namba tatu wa zao la cocoa uliofanyika jumatatu July 15 wilayani humo.

Pamoja na kukamatwa viongozi hao akiwemo mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wilayani Kyela (KYECU) Evance Mwaipopo pamoja na Meneja wa chama hicho Julius Mwankenja, Homera ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Mbeya, kuchunguza chama hicho mifumo yao ya kifedha huku akisitisha taratibu zote za manunuzi Hadi pale kamati ya ulinzi na usalama itakapo jiridhiaha.

Awali akiwasilisha taarifa Kwa mkuu wa Mkoa, mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe Josephine Manasi, amesema hasara hiyo imeonekana baada ya mnunuzi aliyeshinda mnada namba tatu kubaini magunia zaidi ya 200 hayopo kwenye maghara kati ya magunia 1,915 yaliyoshindanishwa kwenye mnada huo.